Story by Rasi Mangale –
Huku zoezi la usajili wa wapiga kura likiendelea kote nchini wakaazi wa kaunti ya Kwale wamehimizwa kutopuuza zoezi hilo na badala yake kujitokeza na kujisajili.
Kinara wa walio wachache katika bunge la kaunti ya Kwale Ndoro Mweruphe amesema kujitokeza kwa wananchi na kujisajili kama wapiga kura ndio njia pekee ya kuchagua uongozi bora na maendeleo mashinani.
Mweruphe ambaye pia ni Mwakilishi wa wadi ya Mkongani amedai kwamba wananchi wanafaa kutumia muda uliotengwa na Tume huru ya uchaguzi na mipika nchini IEBC kushiriki zoezi hilo.
Wakati huo uo amedokeza kwamba kama viongozi wataendeleza hamasa kwa wananchi mashinani kutambua umuhimu wa kujisajili kama wapiga kura.