Story by Hussein Mdune –
Mwanaharakati wa maswala ya kijamii katika eneo la Samburu/chengoni Emmanuel Kadudze Ndaro amewahimiza wakaazi wa eneo hilo na kaunti ya nzima ya Kwale kujitenga na wanasiasa wenye nia ya kuwagawanya katika misingi ya dini na ukabila.
Akizungumza na wakaazi wa eneo hilo, Kadudze amesema wakati huu ambapo kampeni za uchaguzi mkuu zimepamba moto ni lazima kila mmoja kuwa makini dhidi ya semi za viongozi ili eneo hilo lishuhudie amani na maendeleo.
Kadudze ambaye ametangaza nia yake ya kuwania kiti cha uwakilishi wadi wa Samburu/Chengoni amewata wakaazi wa wadi hiyo kuzidi kudumisha amani sawa na kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa.
Wakati uo huo amewasisitiza wakaazi wa wadi hiyo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usajili wa wapiga kura na kujiandikisha kama wapiga kura ili wapate nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu ujao.