Story by Bakari Ali –
Wakaazi wa eneo la Barawa-Utange eneo bunge la Kisauni kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kitaifa na ile ya Mombasa kuingilia kati mzozo wa ardhi ya ekari 3 unaoendelea baina yao na bwenyenye mmoja.
Wakizungumza na Wanahabari baada ya ubomozi wa nyumba zao uliyotekelezwa na watu wasiojulikana waliokuwa wameandamana na maafisa wa usalama wakaazi hao wamesema ni sharti serikali hizo mbili kuibuka na suluhu.
Kwa upande wake Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo amesema wakaazi wa eneo hilo hawatabanduka katika kipande hicho cha ardhi na kuitaka serikali kuangazia suala hilo kwa haki na usawa.
Wakati uo huo Mwanaharakati wa kisiasa katika kaunti hiyo Shafi Makazi amewakashfu viongozi wa kaunti ya Mombasa kwa kutozingatia maslahi ya mwananchi.