Picha kwa Hisani –
Wakaazi wa Ukanda wa Pwani wamehimizwa kusimama kidete na kuitetea ardhi yao kutonyakuliwa na mabwenyenye.
Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amesema wakaazi wa mpwani wameishi kama maskwota kwa miaka mingi, huku wakenya katika maeneo mengine ya nchi wakikabidhiwa hati miliki za ardhi kila uchao.
Ali amesema ni jambo la aibu kwa Serikali kuwapuuza wapwani hasa katika maswala ya ardhi, akiwataka wapwani kutolegeza kamba katika kupigania haki zao za ardhi.
Wakati uo huo, amehimiza usawa katika ugavi wa raslimali sawa na hati miliki za ardhi kwa Mpwani.