Picha kwa hisani –
Familia 12 katika kijiji cha Tumbe huko Msambweni kaunti ya Kwale, wamekosoa hatua ya serikali ya kitaifa na ile ya kuanti ya kwale kwa Kuendeleza Ujenzi Wa Taasisi Ya Utabibu KMTC Katika kijiji hicho.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Salim Pato, wakaazi hao wamesema wameshangazwa na hatua ya serikali ya kuzungushia ua kijiji hicho na kuanzisha ujenzi wa taasisi hiyo bila ya ya kuwapatia ardhi mbadala.
Wakazi hao wanaoishi na makovu ya ukoma wanasema kuwa hali ya maisha imekua ngumu kwao tangu serikali kuzungusha uwa kijiji chao na kuzuiliwa kutoka na kuingia katika kiiji hicho.
Waakazi Hao sasa Wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta Pamoja Gavana Wa Kwale Salim Mvurya, Kuwatafutia Sehemu Mbadala Ili Kuendeleza maisha yao.