Picha kwa hisani –
Idara ya kuhifadhi wanyamapori KWS kaunti ya Taita Taveta, imeshtumiwa vikali na wakaazi wa eneo hilo kwa utepetevu wa kazi, hali inayohatarisha maisha yao na mifugo sawia na mimea yao.
Wakiongozwa na gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja wakaazi hao wamelilaumu shirika la KWS kwa kutowajibika ipasavyo pia kwa kuwadhulumu wakaazi bila kuwapa msaada wowote hususan wanaochoma makaa.
Haya yanajiri huku wanyamapori wakiendela kuwahangaisha wakaazi wa kaunti hiyo, kwa kushambulia mimea shambani mwao sawa na kuhatarisha maisha yao binafsi.