Story by Mwanaamina Fakii –
Wakaazi wa eneo la Silaloni kaunti ndogo ya Samburu katika kaunti ya Kwale Kwale wameitaka serikali na wahisika mbalimbali kuwasaidia kwa maji safi ya matumizi.
Wakaazi hao wamedai kupitia hali ngumu ya maisha kufuatia kushuhudiwa kwa kiangazi kikali katika eneo hilo hali ambayo imewalazimu kutembea mwendo mrefu kutafuta maji.
Wakaazi hao wakiongozwa na Hashim Kazuma Randu wamesema kwa sasa mifugo wao wamefariki kufuatia ukosefu wa maji na chakula kwa mifugo wao.
Kwa upande wake Joyce Kazungu mmoja wa wakaazi wa eneo hilo ameitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kwale kuwatambua wakaazi hao na kuwekeza kina mbinu ili kuwasaidia na maji na chakula.