Story by Janet Shume-
Wakuu wa usalama katika gatuzi dogo la Shimba hills wametoa tahadhari dhidi ya watakaoendeleza hafla za disco matanga nyakati za usiku hususan wakati wa likizo ndefu ya Disemba kwamba watachukuliwa hatua.
Naibu Kamishna eneo hilo Moses Karuige amesema disco matanga zimekua kikwazo kikuu katika jitihada za kutokomeza masuala ya mihadarati, mimba na ndoa za mapema miongoni mwa wanafunzi eneo hilo.
Kwa upande Naibu Chifu mpya wa eneo la Kizibe Ali Abdhalla Bemwendo, ameahidi kushirikiana na wazee wa nyumba kumi pamoja na wazee wa mitaa kuhakikisha masuala hayo yanakomeshwa eneo hilo.