Wakaazi katika eneo la Rabai na kaunti ya Kilifi wamehimizwa kupanda miti katika taasisi sawa na katika maeneo yao ya makaazi ili kutunza mazingira.
Akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Amani,waziri wa utamaduni Mourine Mwangovya amesema amesema ni kupitia njia hio ndipo wananchi wa kaunti hio watakabili baa la njaa ikizigatiwa kuwa miti usaidia katika kuleta mvua ya kutosha.
Kauli yake imejiri baada ya mzee wa kaya kambe Erustus Mrira Kubo kulalamikia uharibifu wa misitu ya kaya hasa katika eneo la Rabai.