Picha kwa hisani –
Wakaazi wa Kaunti ya Taita Taveta na Pwani kwa jumla wamepewa wito kukoma kuuza ardhi zao na badala yake kuzitumia kwa njia ya kujiendeleza pamoja na kurithisha kizazi kijacho .
Akizungumza na wanahabari mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime amewakosoa baadhi ya wakaazi wa Taita Taveta ambao bado wanaendelea kuuza ardhi zao licha ya eneo hilo kukubwa na changamoto ya ardhi .
Wakati uo huo Mwadime amewashauri wakaazi wanaoishi maeneo ya Milimani na wanamiliki mashamba sehemu za za chini kuyatumia kwa shughuli ya ukulima na pia kubuni makao yao.
Aidha licha ya tatizo la umiliki wa ardhi kuwa donda sugu katika eneo la Pwani suala la umaskini limechangia wengi wa wakaazi kuuza ardhi zao kwa thamani ya chini .