Picha kwa hisani –
Wakaazi wa eneo la pwani wametakiwa kuviunga mkono vyama vya kisiasa vya Pwani ili kuleta mabadiliko katika eneo hilo.
Kulingana na mwenyekiti wa chama cha Umoja Summit Party of Kenya katika kaunti ya Kilifi Birya Menza, wanasiasa wengi katika eneo hilo wamevipa kipaumbele vyama vya kutoka nyanja za juu hali ambayo imeregesha nyuma maendeleo ya pwani.
Birya amewataka viongozi wa pwani kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili pwani iweze kuboreka kimaendeleo.
Wakati huo huo ameongeza kuwa ni sharti nakala za ripoti ya BBI ziletwe mashinani ili mwananchi aweze kuisoma na kuielewa vyema ripoti hiyo, badala ya kuwaitisha wananchi sahihi.