Picha kwa Hisani –
Tangu eneo la Pwani lipokee jumla ya kadi elfu 150 za huduma namba, idara ya usajili wa watu katika eneo la Pwani imekuwa ikijizatiti kuwawezesha wananchi kuzichukua kadi hizo.
Msajili mkuu wa watu katika eneo la Pwani Aggrey Masai amewarai wakaazi waliopata ujumbe mfupi kwenye simu zao za rununu kuhusu kadi hizo kujitokeza na kuzichukua.
Akizungumza alipokagua zoezi la kutoa kadi hizo katika jumba la Posta Kisiwani Mombasa, Masai amesema wakaazi wanajitokeza kwa mwendo wa kinyonga kuzichukua kadi hizo.
Wakati uo huo, amefichua kuwa imewalazimu Maafisa wa Idara hiyo kuzuru mashinani ili kuwafikishia wananchi wenyewe kadi zao.