Picha kwa hisani –
Jumla ya familia 3,200 zinazoishi katika ardhi inayokabiliwa na mzozo ya Nguu tatu katika eneo la Kisauni kaunti ya Mombasa wameandamana na kupiga kambi nje ya afisi ya Mbunge wa eneo hilo Ali Mbogo wakitaka Mbunge huyo kuwapatia makao.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Robert Nugo, wakaazi hao wamewakosoa mabwenyenye wanaodai umiliki wa ardhi hiyo ya ekari 589, wakisema wamevamiwa na Maafisa wa polisi usiku wa kuamkia leo na kupigwa.
Kulingana na Nugo, kesi hiyo ingali mahakamani na wakaazi hao waliruhusiwa na Mahakama ya Shanzu kuishi kwenye ardhi hiyo hadi kesi hiyo iamuliwe.
Kwa upande wake, mmoja wa wakaazi hao Bi Ngoze Mwambazi amesema wakaazi hao wameteseka katika ardhi hiyo, huku wakiapa kutoondoka kwenye kipande hicho cha ardhi.
Hadi hii leo jioni, familia hizo zilikuwa zimepika chakula nje ya afisi ya Mbunge huyo na kutandika mikeka yao wengine wakilala, huku Maafisa wa polisi wakisalia kuwatazama.