Story by Gabriel Mwaganjoni –
Zaidi ya familia 200 zilizoathirika na ubomozi wa nyumba za makaazi katika eneo la Mwamdudu katika gatuzi dogo la Kinango kaunti ya Kwale sasa zinadai kwamba bwenyenye mmoja aliwahadaa baadhi ya wakaazi na kuinyakua ardhi hiyo.
Wakiongozwa na Ramadhan Lewa, wakaazi hao wameitaka Serikali kuingilia kati ili waipate ardhi yao huku wakimshinikiza Rais Uhuru Kenyatta kuchukua hatua za kisheria.
Kulingana na Lewa, Afisa mmoja wa ngazi ya juu Serikalini alishirikiana na mwekezaji mmoja ili kuwanyang’anya ardhi yao wakaazi hao.
Kwa upande wao, baadhi ya wakaazi akiwemo Mwanamisi Ramadhan na Salama Kenga wamedhihirisha masikitiko yao kufuatia dhuluma hiyo.