Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wakaazi wanaotumia daraja la Nyali kuelekea upande wa Mombasa Kaskazini au Kisiwani Mombasa wamedhihirisha wasiwasi wao kufuatia kuharibika kwa daraja hilo na kukosa kurekebishwa.
Kulingana na wakaazi hao, tangu gari dogo kupata ajali katika daraja hilo majuma mawili yaliopita na kubomoa baadhi ya vizuizi katika daraja hilo, bado vizuizi hivyo havijajengwa upya.
Wakizungumza katika daraja hilo, wakaazi hao wamewataka wahusika kukarabati sehemu iliyobomolewa kabla ya ajali nyingine kutokea katika eneo hilo.
Hata hivyo wamewapa wahusika mda wa hadi siku ya Jumatatu iwe daraja hilo limekarabatiwa.