Wakaazi wa Kaunti ya Mombasa wamezidi kuhimizwa kuchukua tahadhari wakati huu mvua inapoendelea kunyesha ili kuzuia majanga.
Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema kwamba japo kaunti hiyo imekuwa ikipokea viwango vya chini vya mvua, ni lazima wakaazi hasa wale wanaoishi kwenye maeneo ya mabonde kuchukua tahadhari.
Achoki amekariri kwamba mipangilio imewekwa ili kuikabili hali yoyote ambayo itahatarisha maisha ya wakaazi iwapo Kaunti hiyo itashuhudia mafuriko.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.