Story by Ngombo Jeff-
Kufuatia kuongezeka kwa visa vya dhulma za kijinsia dhidi ya watoto katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, sasa wakaazi wa eneo hilo wamefanya maandamano kushinikiza kukomeshwa vya visa hivyo.
Wakaazi hao wakiongozwa na Wanahakati wa kijamii wamedai kwamba visa hivyo vimekithiri mno na kuwaathiri watoto wa umri mdogo wa chini ya miaka 15.
Wamesema kisa cha hivi punde cha afisa mmoja wa polisi kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 15 ni aibu mno katika jamii wakitaka afisa hyo wa polisi kuchukuliwa hatua kali za kisheria huku wakidai kuchukizwa na tabia hiyo sawa na kuwalaumu maafisa wa polisi ambao wanakiuka haki za binadamu na kuwanyanyasa watoto.