Wakaazi wa maeneo ya Aldina-Mikanjuni katika eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wameanza kujikarabatia barabara wenyewe kufuatia mahangaiko wanayopitia hasa kunapotokea dharura.
Wakaazi hao wakiongozwa na Mwanaharakati wa kijamii Nicholas Kisera, wamesema wamekuwa wakichangisha fedha ili kuanza ujenzi wa barabara hizo baada ya Serikali ya kaunti ya Mombasa kupuuza kilio chao.
Mmoja wa wakaazi hao Lillian Mwawira amesema wametaabika sana huku tatizo hilo likiwahangaisha zaidi pindi kunaponyesha.
Akikiri kuwepo kwa hali hiyo, Mwakilishi wa Wadi ya Mikindani Juma Renson Thoya ameitaja hali ya miundo msingi katika Wadi hiyo kama ya kusikitisha, akitaka barabara zote katika eneo hilo zikarabatiwe