Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Lungalunga kwa tiketi ya chama cha UDM Mangale Chiforomodo amewataka wanasiasa kukoma kueneza siasa za chuki na uchochezi miongoni mwa wakaazi.
Akizungumza wakati wa mikutano yake ya kisiasa katika eneo bunge la Lungalunga, Mangale amesema siasa za migawanyiko ya kikabila hazijengi bala huchangia uhasama miongoni mwa jamii.
Mwanasiasa huyo amewataka viongozi wa kisiasa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kueneza ujumbe wa amani, akisema hatua hiyo ndio itakayochangia taifa hili kushuhudia uchaguzi wa amani.
Wakati uo huo amehimiza umuhimu wa wakaazi wa kaunti ya Kwale kujitenga na wanasiasa wachochezi na badala yake kuwachagua viongozi wenye malengo ya maendeleo.