Wizara ya ardhi nchini imewakabidhi wakaazi wa Vyemani eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa,zaidi ya hati miliki elfu moja za ardhi zao.
Afisa katika wizara ya ardhi nchini Sammy Mchombo amesema kuwa ugavi wa hati miliki kwa wakaazi kutasaidia kupunguza migogoro ya ardhi inayoshuhudiwa mara kwa mara katika eneo bunge hilo.
Kwa upande wake kamishina wa kaunti ya mombasa Evans Achoki amewataka wakaazi eneo hilo ambao hawajachukua hatimiliki zao kujitokeza kwa idara husika na kuchukua vyeti hivyo.
Hata hivyo amewasihi wakaazi wa Mombasa kujitenga na tabia ya kuuza mashamba yao kiholela.
Taarifa na Hussein Mdune.