Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wafanyiabiashara, watetezi wa haki za kibinadamu, mashirika ya kijamii, wadau katika sekta ya elimu na wakaazi wa Lamu wamezuru katika bandari ya Lamu kwa mara ya kwanza na kufanya kikao eneo hilo.
Kikao hicho kimeongozwa na Kamishna wa kaunti hiyo Irungu Macharia kinalenga kuwapatia wakaazi hao fursa ya kuzuru mradi huo wa mabilioni ya pesa sawia na kutoa mapendekezo yao ili yakabidhiwe Serikali.
Macharia amesema mradi huo unapaswa kuinua jamii ya Lamu kikamilifu sawia na kuwashirikisha wakaazi hao katika nafasi mbalimbali zitakazotokana na mradi huo mkubwa wa kiuchumi.
Wakaazi hao wamesema tayari dalili za ubaguzi katika nafasi za ajira miongoni mwa wakaazi wa kaunti hiyo zimeonekana, wakitaka hali hiyo kukomeshwa na wakaazi kupewa kipau mbele.