Mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti ya Kwale Dominick Mbindyo amewataka wakaazi kuchukua tahadhari kipindi hiki ambapo mvua za masika zinatarajiwa kuanza ili kuepuka athari za mafuriko.
Akiongea mjini Mombasa Mbindyo amesema mvua hizo zinazotarajiwa kuanza mwezi huu zitanyesha kwa kiwango cha kati ya mililita 350 hadi mililita 450.
Wakati uo huo amewataka wakulima katika kaunti hiyo kujitenga na mbinu za kilimo za kitamaduni na badala yake wakumbatie kilimo cha kisiasa ili wanufaike.
Taarifa na Hussein Mdune.