Story by Hussein Mdune
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kutoa ufadhili kwa watoto la Compassion National Kenya Samuel Wambugu amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kuzingatia umuhimu wa utunzi wa mazingira.
Akizungumza katika halfa ya kupanda miti iliyofanyika katika Kanisa la PEFA katika eneo la Maweu kaunti ya Kwale, Wambugu amesema iwapo wakaazi watazingatia upanzi wa miti basi watakabiliana na swala la ukame.
Naye Msimamizi wa Shirika hilo kaunti ya Kwale Ailean Munga amesema kama Shirika tayari wamepanda zaidi ya miti elfu 50 huku akidai kwamba mwaka huu wanalenga kupanda zaidi ya miti mia mbili.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa la PEFA katika eneo ya Mtaa kaunti ya Kwale Peter Mwero amesema kama viongozi wa kidini watahakikisha wanatoa hamasa kwa wakaazi kuhusu umuhimu wa upanzi wa miti.