Naibu Kamishna wa gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale Isaac Keter amewaomba wakaazi wa Kwale kujitayarisha kwa zoezi la kuhesabu watu itakayofanyika rasmi mwaka ujao.
Akiongea na Wanahabari baada ya Sherehe ya maadhimisho ya siku ya takwimu Barani Afrika iliofanyika mjini Kwale, Keter amesema zoezi hilo ni muhimu kwani itaisaidia serikali kupanga mipangilio yake ya maendeleo vyema.
Keter amehoji kuwa mara nyingi zoezi hilo linapoandaliwa watu wengi huogopa kutaja idadi ya watu walio katika familia zao, akisema kuwa wakati huu hakuna majina ya watu yakayotakikana.
Wakati uo huo amedokeza kuwa maafisaa watakaoendeleza zoezi hilo watakuwa na vitambulisho maalum vya kujitambulisha kwa wakaazi hususan mashinani.
Taarifa na Mariam Gao.