Story by Hussein Mdune-
Mgombaye wa kiti cha ubunge wa Kinango kwa tiketi ya chama cha UDM Beja Mwambeyu ameweka wazi kwamba uchaguzi wa Agosti 9 utakuwa wa amani kama wakaazi watajitenga na wanasiasa wachochozi.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa, Mwambeyu amesema kuna baadhi ya viongozi wanaendeleza siasa za kuwagawanya wakaazi hivyo basi kuna haja ya wananchi kuwa makini.
Aidha amewataka wakaazi wa Kkinango na kaunti ya Kwale kwa jumla kujitenga na siasa za ukabila kwani huenda zikachangia siasa za vurugu.
Wakati uo huo amewataka wakaazi kuwachagua viongozi kwa kuzingatia sera zao na wala sio vyama vya kisiasa ili kuwawezesha kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo.