Story by Mwanaamina Fakii –
Waziri wa Afya katika serikali ya kaunti ya Kwale Francis Gwama amewashauri wakaazi wa Kwale kuvitembelea vituo vya afya vilivyoidhinishwa na Wizara ya afya nchini ili kupokea chanjo ya Corona.
Gwama amesema jamii imekuwa ikiendeleza uvumi kuhusiana na chanjo hiyo,akisema sio ukweli huku akisisitiza kwamba chanjo hiyo imepitia uchunguzi wa wataalam wa kiafya na ni salama kwa maisha ya binadamu.
Waziri huyo amewahakikishia wakaazi wa kaunti ya Kwale usalama wa chanjo hiyo huku akiwataka kuondoa wasiwasi na badala yake wajitokeze kupokea chanjo.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba hata baada ya mtu kupata chanjo ya Corona ni lazima aendelee kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.