Story by Salim Mwakazi –
Meneja wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC katika kaunti ya Kwale Nelly Ilongo amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu.
Nelly amesema idadi ndogo ya wakaazi imejisajili kama wapiga kura, akidokeza kuwa kuna haja ya wakaazi kujitokeza kwa wingi ili kuzuia msongamano wa usajili huo wakati wakenya wanapokaribia siku za uchaguzi.
Akizungumza na Wanahabari, Ilongo amesema kufikia sasa ni asilimia 25 pekee ya wakaazi waliojisajili kama wapiga kura katika kaunti ya Kwale kinyume na ilivyotarjiwa.
Hata hivyo, amedokeza kuwa tume hiyo imeanzisha mpango wa kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujisajili huku akisema wanashirikiana na machifu ili kuhakikisha wananchi wanajisajili katika afisi za IEBC.