Story by: Rasi Mangale
Waakazi wa wadi ya Kasemeni na Mwavumbo eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale, wameandamana wakilalamikia kubaguliwa katika utoaji wa ajira na fidia kwenye mashamba yao yaliyochukuliwa na serikali kufanikisha mradi wa bwawa la Mwache.
Wakiongozwa Jackson Mwamvula Dzeha wakaazi hao wamesema fidia ambayo wanalipwa kwa sasa na serikali sawa na wawekezaji wa mradi huo ni shilingi laki tatu na elfu hamsini kwa kila ekari kinyume na makubaliano ya hapo awali ambapo walipaswa kulipwa shilingi milioni moja kwa kila ekari.
Waakazi hao wamemtaka Rais William Ruto kusikiliza kilio chao na kuingilia kati swala hilo ili kuhakikisha matakwa yao yanatatuliwa kikamilifu.
Kwa upande wake Rukia Mshenga amesema ni hali ya kusikitisha kuona wenyeji wa maeneo hayo wakiachwa nje katika swala la ajira hali inayokuika sheria za uajiri kulingana na katiba.
Wakati uo huo Emmanuel Chanze, kijana wa eneo hilo amesema licha ya kuwa na vyeti hitajika vya kumuwezesha kupata ajira kwenye mradi huo wa mamilioni ya pesa wa Bwawa la Mwache bado hajapata nafasi ya ajira.