Taarifa na Sammy Kamande.
Wakaazi wa Kadzandani eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa wameitaka serikali kuu na ya kaunti ya Mombasa kutengeneza mabomba ya kupitisha maji taka katika eneo hilo.
Hii ni baada ya jamaa mmoja mwenye umri wa makamo aliyefahamika kwa jina Hamisi kudaiwa kufariki baada ya kuzama maji yaliyozaga mtaa wa Soweto.
Kulingana na Eunice Bozo mmoja w awakaazi wa eneo hilo, baadhi ya nyumba zimebakia mahame huku akidai maji kufurika na kuingia hadi katika nyumba za wakaazi.
Aidha Bozo amedai chanzo cha kujaa maji katika eneo hilo ni kutokana na mitaro michache ya kupitishia maji ya mvua.