Mgogoro wa ardhi umechipuka upya katika eneo la Jomvu kuu kaunti ya Mombasa baada ya wakaazi kuandamana mapema leo wakidai kuwa ardhi yao kunyakuliwa na Kanisa la Kimethodisti.
Wakaazi hao Wakiongozwa na Mzee wa kijiji hicho Salim Mwidani, wamesema ardhi yao imenyakuliwa na sasa wanaishi katika kipande kidogo cha ekari 6 pekee huku Kanisa hilo likinyakua zaidi ya ekari 155.
Kwa upande wake, Msemaji wa jamii hiyo Ahmed Kombo Ahmed amesema zaidi ya familia elfu 10 za jamii hiyo ya wajomvu zinaishi kwa hofu kwa kushurutishwa kuondoka katika eneo hilo.
Naye Mwanaharakati wa akina mama katika eneo hilo Bi Fatuma Mwinyi amewataka viongozi husika kuzuru eneo hilo na kuutanzua mgogoro huo