Story by Mercy Tumaini –
Wakaazi wa eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi wameshauriwa kujisajili kama wapiga kura ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.
Aliyekuwa Mwakilishi wadi ya Ruruma katika eneo la Rabai, Naphtali Kombo amesema vijana wengi katika eneo hilo hawajajisajili kama wapiga kura na huenda hali hiyo ikachangia kuchaguliwa viongozi wasio na ajenda za maendeleo.
Wakati uo huo amewasihi wanasiasa katika eneo hilo kuendeleza siasa za amani badala ya kueneza chuki na migawanyiko ya kisiasa.