Wakaazi wa eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa wanadai kutengwa na serikali kuu katika masuala yanayohusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo hilo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Ahmed Shahame wakaazi hao wamedai kuwa licha ya serikali kuidhinisha miradi ya maendeleo eneo hilo, jamii haijanufaika kiajira.
Shahame amepiga mfano wa mamlaka ya bandari akiihimiza kuitambua jamii hiyo kwa kutoa ajira kwa vijana wa eneo hilo.
Katiba ya nchi inazitaka kampuni zinazohudumu katika maeneo mbali mbali nchini kutoa nafasi za ajira kwa jamii ya maeneo hayo.
Taarifa na Hussein Mdune.