Story by Bakari Ali-
Wakaazi wa eneo la Bangladesh gatuzi dogo la Jomvu kaunti ya Mombasa wameilaumu serikali ya kaunti ya Mombasa kwa kutotilia maanani suala la uhaba wa maji.
Wakizungumza na Wanahabari, wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na Caroline Auma, wameikashfu serikali ya kaunti hiyo kwa kutoangazia kwa kina suala hilo ambalo limedumu kwa mda mrefu.
Akiunga mkono kauli hiyo Dorcas Dhahabu ambaye pia ni mkaazi wa eneo hilo ameitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati suala hilo kwani uhaba wa maji katika eneo hilo imekuwa changamoto kuu.
Kwa upande wake, Kaimu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya usambazaji maji ya Mombasa Abdulrahim Farah amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuwa na subra kwani swala hilo linashuhulikiwa.