Story by Ephie Harusi
Wakaazi wa wadi ya Bamba katika gatuzi ndogo ya Ganze kaunti ya Kilifi wamelalamikia kushuhudiwa kwa uhaba wa maji katika eneo hilo licha ya kuwepo na serikali ya ugatuzi.
Wakaazi hao wakiongozwa na Stephen Rimba Gona wamesema serikali ya kaunti hiyo imeshindwa kuwajibikia majukumu yake na kuchangia wakaazi wa eneo hilo kuhangaika kila siku kutafuta bidhaa hiyo muhimu.
Gona amesema wakaazi wa eneo hilo wanalazimika kununua bidhaa hiyo kwa shilingi 70 hadi 100 kwa mtungi wa lita 20.
Kauli yake imeungwa mkono na Anderson Kenga Jefwa aliyesema wakaazi wa eneo hilo hulazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta bidhaa hiyo muhimu hata zaidi ya kilomita 15.