Picha kwa hisani –
Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadam pamoja na wakaazi wa kaunti ya Kwale wameandamana wakilalamikia huduma duni kutoka kwa kampuni ya usambazaji umeme katika eneo hilo.
Wakiongozwa na Mahmoud Baro wanaharakati hao wamesema kumeshuhudiwa msururu wa mikasa na maafa ya wakaazi yanayochangiwa na nguvu za umeme kutokana na utepetevu wa maafisa wa kampuni hio.
Hata hivyo maafisa wa polisi wamefika eneo la Tiwi ambako maandamano hayo yameanzia na kuamrisha kwamba ni watu 15 pekee wanaoruhusiwa kushiriki maandamano hayo ambayo yalioelekea hadi afisi za kampuni ya kusambaza umeme eneo la Ukunda hatua ambayo haikuridhisha waandamanaji hao.
Maandamano hayo yamejiri siku chache baada ya mama mmoja na mwanawe wa miezi mitatu kuaga dunia baada ya kupigwa na nguvu za umeme katika eneo la Bowa huko Kombani, Kwale.