Picha kwa hisani –
Wakaazi katika eneo la Rabai kaunti ya Kilifi wameandamana mapema leo hadi katika afisi za idara ya maji eneo la Mazeras wakitaka kuelezwa kiini cha uhaba wa maji unaokumba eneo hilo.
Wakiongozwa na aliyekuwa seneta maalum Bi Emma Mbura,wakaazi hao wakiwemo wahudumu wa bodaboda wamelalamikia uhaba wa maji wakitaka hali hiyo isuluhishwe.
Kulingana na Mbura,wamekuwa wakiuziwa maji kwa gharama kubwa ya hadi shilingi 100 kwa mtungi wa lita 20.
Kwa sasa Mbura anamtaka Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Jeffa Kingi kuisuluhisha hali hiyo ili kuwawezesha wakaazi hao wa Rabai na maeneo ya Chonyi kupata huduma za maji.
Wakaazi hao wameapa kuandamana kila siku hadi tatizo hilo litakapotanzuliwa.