Picha kwa Hisani –
Wakaazi katika eneo Hindi kaunti ya Lamu wameitaka wizara ya mazingira ya kaunti hio kusitisha uchimbaji mchanga unaoendelezwa katika mtaa wa Safiris ndani ya eneo hilo.
Wakiongozwa na balozi wa nyumba kumi Moses Kariuki wakaazi hao wamesema uchimbaji mchanga unaoendelezwa umeathiri shughuli za kilimo kutokana na vumbi kali linalotoka kwenye timbo za mchanga.
Kwa upande wake Philister Wangare mmoja wa wakaazi eneo hilo amesema mbali na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli hizo za uchimbaji madini wakaazi wako katika hatari kupata madhara ya kiafya.