Picha kwa hisani –
Kumeshuhudiwa purukushani la kisiasa katika bunge la kaunti ya Baringo wakati wa hoja ya kuujadili mswada wa BBI uliowasilishwa bungeni humo.
Mvutano huo wa kisiasa kati ya Wawakilishi wa wadi wa chama cha Jubilee na KANU ulianza pale Mwakilishi wa Wadi ya Kabarnet Ernest Kibet, na Mwenzake wa Magotio Charles Kosgei kutofautia kisiasa kuhusu yaliomo ndani ya BBI.
Ilimlazimu Spika wa bunge la kaunti hiyo David Kiplagat kuingilia kati mvutano huo na kuutuliza baada ya viongozi hao tayari walikuwa wamezibana Makonde bungeni humo.
Tayari bunge la kaunti ya Siaya, Kisumu na Homabay kutoka eneo la Nyanza zimeupitisha mswada huo wa BBI na kuwasilisha ripoti ya kuidhinishwa kwa mswada huo mbele ya bunge la Kitaifa na lile la Seneti.