Wajumbe wa bunge la kaunti ya Kwale wanataka kushirikishwa katika miradi yote inayoidhinishwa katika kaunti hiyo.
Katika mahojiano na meza ya muliko mwakilishi wa wadi ya Waa/Ngombeni Mwinyi Mwaserah amesema kwamba hawapingi miradi inayoidhinishwa bali wanataka kushirikishwa ili kutoa muongozo wao kwa manufaa ya wananchi.
Kauli yake inajiri baada ya bunge la kaunti ya Kwale kupitisha mswada wa kusimamisha mradi wa bwawa la Mwache ili wafahamu kwanza faida zake kwa mwananchi wa Kwale.
Mwaserah amesema kwamba si vyema kwa bunge la kaunti ya Kwale kukosa kushauriwa kuhusiana na mradi huo wa serikali kuu.
Taarifa na Salim Mwakazi.