Story by Our Correspondents-
Mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Roots Party Prof George Wajackoyah, amevikosoa vyombo vya habari nchini kwa kuangazia kampeni za wanasiasa kwa njia ya upendeleo.
Wajackoyah amevitaka vyomba vya habari nchini kuzingatia usawa na uwazi katika utendekazi wao ili kuhakikisha taarifa zinazoperushwa hewani zinaangazia sera za wanasiasa wote hasa ngazi ya urais.
Akizungumza katika Kongamano la siku nne la kuangazia maandalizi ya uchaguzi mkuu lililoandaliwa na Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi, Wajackoyah amesema chama cha Roots Party kiko tayari kwa uchaguzi mkuu na wala hakiwezi kumkejeli mwanasiasa yeyote.
Mgombea huru wa kiti cha urais wa Agosti 9, amewataka viongozi wa kidini kutozikosoa sera zake na badala yake kushirikiana naye ili kurekebisha mahali ambapo wanahisi wanajaridhishw na wala sio kumkejeli kila uchao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, amesema tayari tume hiyo imepiga hatua katika kufanikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu huku akidokeza kwamba maafisa wa tume hiyo wamejiandaa vyema.