Story by: Abdallah Mwanyiro
Waumini wa dini ya Kiisalam katika kaunti ya Lamu wamehimizwa kutojihusisha na tabia zisizofaa wakati wanapojiandaa kuanza funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Kadhi wa Lamu Swaleh Mohamed Ali amesema mara nyingi watu huangazia zaidi kurembesha majumba na kununua vyakula wakati ramadhani inapokaribia huku wakisahau mambo muhimu ya ibada inavyopasa kufanywa.
Aidha amesema swala la watu kuenda katika fukwe za bahari hindi na kujivinjari kwa madai ya kuupokea mwezi wa Ramadhani ni kinyume na sheria kwani mara nyingi watu hufanya maasi ya kutangamana kwa wanawake na wanaume.
Hata hivyo amedai kwamba haina haja ya watu kuzozana kutokana na kutofautiana kwa kuandamwa kwa mwezi akisema kila mtu ana haki ya kisheria kufuata msimamo wake juu ya muandamo wa mwezi na lazima waheshimiane.