Wahudumu wa afya katika hospitali ya umma ya King Fahad Kaunti ya Lamu wanaendeleza mgomo baridi kwa kile wanachokidai kama kupuuzwa na Serikali ya Kaunti hiyo.
Tayari watetezi wa haki za kibinadamu waliyozuru hospitali hiyo wakiongozwa na afisa mkuu wa shirika la Haki Afrika Yunus Isaack Ahmed wamezidi kuishinikiza serikali ya kaunti hiyo kuiwajibikia sekta ya afya kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.
Yunus amesema, wagonjwa waliyozuru hospitali hiyo hii leo kusaka huduma za matibabu wamelazimika kurudi nyumbani bila ya kuhudumiwa.
Kwa sasa Yunus anataka mwafaka wa dharura kati ya wahudumu hao na Serikali ya Kaunti ya Lamu kwani kulingana na watetezi hao kilio cha wahudumu hao ni cha haki.
Baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali hiyo ambao wameambukizwa virusi vya Corona wangali majumbani wakiendelea kujitenga.