Chama cha wahudumu wa Tuk Tuk kaunti ya Mombasa kimekanusha madai kuwa wahudumu wa Tuk Tuk wanijihusisha na uhalifu.
Kulingana na mwenyekiti wa chama hicho Obedi Muruli mara nyingi wanaotekeleza uhalifu sio wahudumu wa Tuk Tuk bali ni watu wanaojifanya kuwa wahudumu.
Hata hivyo Muruli amewataka watumizi wa Tuk Tuk kushirikiana na wahudumu kutoa ripoti za watu wanaofanya uhalifu kwa kutumia Tuk Tuk ili wakabiliwe kisheria.
Mwenyekiti huyo wa wahudumu wa Tuk Tuk amewahimiza kuwa waangalifu barabarani hususan kipindi hiki cha likizo ya mwisho wa mwaka.
Taarifa na Hussein Mdune