Wahudumu wa matatu hapa Pwani hawatarudi barabarani hadi pale utata unaozunguka sheria ya mraba wa manjano kwenye matatu utakapotatuliwa.
Mshirikishi wa chama cha wamiliki wa matatu kanda ya pwani Salim Mbarack Salim amesema waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i na mwenzake wa uchukuzi James Macharia wamehitilafiana pakubwa na sheria za uchukuzi wa umma.
Mbarack amesema iwapo utata huo utatatuliwa kufikia leo jioni kwenye mkao wa majadiliano unaofanyikaa kule jijini Nairobi basi shughuli za uchukuzi wa umma zitaregea katika hali yake ya kawaida.
Mbarack hata hivyo amelitaja swala la michoro na picha zinazopachikwa kwenye magari ya umma kama lisilostahili kuingizwa utata wowote wala maafisa wa trafiki kutolitumia kama kigezo cha kuzinasa matatu, akisema rais Uhuru Kenyatta aliwaruhusu wamiliki hao kuwaajiri vijana waliyo na talanta katika kuzirembesha matatu.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.