Wahudumu wa maboti ya uchukuzi wa abiria katika mkondo wa Bahari hindi wa Ganaola huko Mikindani Kaunti ya Mombasa./Picha Gabriel Mwaganjoni.
Wahudumu wa maboti ya uchukuzi wa abiria katika mkondo wa Bahari hindi wa Ganaola huko Mikindani Kaunti ya Mombasa wametakiwa kutumia vifaa maalum vya usalama pindi wanapoendeleza shughuli zao za uchukuzi baharini.
Kiongozi wa kijamii wa eneo hilo Wanje Ziro amezema manahodha na abiria wao hupuuza kuvaa makoti maalum ya usalama sawia na kuzingatia maswala mengine muhimu ya kuzuia mikasa katika bahari hindi.
Akizungumza huko Ganaola mapema leo, Mzee Ziro amehoji kwamba mikasa inayoshuhudiwa katika eneo hilo ya maboti kupinduka mara nyingi inatokana na uendeshaji wa maboti hayo kiholela na kuwabeba abiria kupitia viwango hitajika ili kuwavukisha hadi upande wa Rabai Kaunti ya Kilifi.
Ziro ametaka abiria kulazimishwa kuvalia makoti hao ya usalama, maboti hayo kuzuiliwa kuwabeba abiria kupata kiasi, na maboti hayo kukaguliwa ili kubaini iwapo yako katika hali nzuri.
Kauli ya Ziro inajiri siku mbili tu baada ya mwanamume mmoja kufariki baada ya kuzama maji kufuatia mkasa wa boti katika eneo hilo la Ganaola huko Mikindani Kaunti ya Mombasa.