Picha kwa hisani –
Wahudumu wa bodaboda katika eneo la Bamburi Kaunti ya Mombasa wana muda wa majuma mawili kuhakikisha wana vibali vyote hitajika vya kutekelezea kazi hiyo la sivyo wapambane na mkono wa sheria.
Naibu kamishna anayesimamia Tarafa ya Bamburi Bi Pamela Akinyi amesema sekta hiyo ni muhimu mno kwa uchumi wa nchi na usalama vile vile na haiwezi kutelekezwa.
Akizungumza huko Bamburi hii leo, Bi Akinyi amesema ni lazima wahudumu hao wa Bodada wawe na leseni na makoti maalum yaani reflectors sawia na kofia maalum yaani helmet ili kuwakinga na majeraha endapo watahusika kwenye ajali.
Hata hivyo, Afisa huyo tawala amesema wahudumu hao watapewa hadi mwezi Februari mwakani kuainisha sheria na katiba yao kuhusiana na shughuli za uchukuzi wa boda boda.