Story by Gabriel Mwaganjoni-
Ni sharti wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Mombasa wajisajili katika mpango wa bima ya kitaifa ya afya NHIF ili wanufaike na huduma za matibabu katika hospitali za umma nchini.
Kulingana na mgombea wa ugavana wa kaunti ya Mombasa Mhandisi Mkalla Chitavi, wahudumu wa bodaboda wamechangia pakubwa kuimarika kwa uchumi wa kaunti hiyo na ni sharti maslahi yao yazingatiwe kikamilifu.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Chitavi ametaka wasimamizi wa hazina hiyo katika kaunti ya Mombasa kuhakikisha wanawahamasisha wahudumu hao kuhusu umuhimu wa bima hiyo ili kulinda afya zao.
Chitavi amekiri kwamba wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Mombasa wanateseka hasa katika maswala ya afya ikilinganishwa na kaunti nyingine za Pwani.