Picha kwa hisani –
Mgomo wa wauguzi na maafisa wa kliniki katika kaunti ya Mombasa umechukua mkondo tofauti baada ya wahudumu hao wa afya kuapa kuanzisha kampeni za kuipinga BBI
Wakiongozwa na Katibu wa Muungano wa maafisa wa kliniki katika kaunti hiyo Frankline Makanga,wahudumu hao wamesema watawarai wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuupinga mchakato wa BBI hadi pale matakwa yao yatakapotimizwa.
Makanga amesema tayari wahudumu hao wanaendeleza kampeni ya kuwarai wakaazi wa kaunti hiyo kutoshiriki vikao vya BBI.