Picha kwa hisani –
Miungano mbali mbali ya wahudumu wa afya nchini ikiwemo madaktari,wauguzi maafisa waabara imetoa ilani ya kuanza mgomo kuanzia saa sita usiku hii leo.
Katibu mkuu wa chama cha maafisa wa afya ya umma nchini Mohamed Duba amesema wizara ya afya nchini imeshindwa kutekeleza mapendekezo yao ya kuwapandisha vyeo.
Duba amesema wahudumu wa afya katika vituo vyote vya umma watashiriki mgomo huo,ikiwemo wale wanaohudumu katika viwanja vya ndege,mipakani sawa na kwenye hifadhi za damu.
Amesema licha ya wahudumu wa afya kutoa mapendekezo yao kwa wizara ya afya mapema mwezi mei mwaka huu,usimamizi wa wizara hio umepuuza kilio cha wahudumu wa afya.