Story by Ali Chete –
Wahudumu wa Afya katika kaunti ya Mombasa wamedai kutorudi kazini hadi pale serikali ya kaunti hiyo itakapotekeleza matakwa yao huku mgomo huo ukiingia siku ya tatu.
Wahudumu hao wakiongozwa na Katibu chama cha maabara katika kaunti hiyo Moses Maingi wamesema hawatarudi kazini na kuitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kukoma kutoa vitisho kwa wahudumu hao.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Muungano wa wataalum wa afya nchini tawi la Mombasa Ben Katana, ameitaka serikali ya kaunti hiyo kuwalipa wahudumu hao mishahara yao ya miezi miwili pamoja na kuwalipia ada wanazotozwa na benki za muda wa miezi 5.
Kauli zao zimeungwa mkono na Naibu Mwekahazina wa Muungano wa madaktari nchini KMPDU kanda ya Pwani Dkt Mariam Mwajumla ambaye amewalaumu viongozi wa kaunti hiyo kwa kukosa kuangazia maslahi yao.